Scroll To Top

Mungu Ana Mpango

Sehemu ya Pili ya Mfululizo huu

Na Jacquelyn Fedor

Ilitafsiriwa Na David Odhiambo
2010-04-19


Tafadhali bofya maandishi ya samawati hafifu kwa maelezo zaidi


Bwana alionekana kwa watu wake kwa siku 40 baada ya kufufuka kwake ili ushindi wake uweze kuonekana na kurekodiwa kwa vizazi vitakavyofuata. Kisha akapaa mbinguni, akiacha karama za Waefeso 4:11 kwa kanisa ili kuinua mwili tofauti kwa ajili yake. Watu hawa waliozingatia umoja watakuwa kimo chake kamili, mwili ambao Roho Wake ataishi ndani yake ili kuleta urejesho na ushindi duniani kimwili. Kama tulivyoona katika sehemu ya kwanza, changamoto ambayo Yesu alikabili msalabani na ushindi wake dhidi ya kifo, kuzimu na kaburi ulibadilisha mambo kwa kiasi kikubwa katika ulimwengu wa roho kwani vita vyake dhidi ya roho. Lakini kumbuka, Yeye pia alipigana kama nyama na damu, mwanadamu, na kwa nafasi akawezesha mabadiliko hapa duniani. Alipigana na kumshinda mtawala wa giza aliyejitangaza kuwa mungu wa sayari hii. Kisha Neno akapaa hadi nyumbani kwake mbinguni yule mshindi.
Hivyo Kristo alisuluhisha swali hilo mara moja na kwa wote, ambaye alikuwa Bwana wa Mabwana mbinguni na hapa duniani. Ushindi wake ulitambuliwa mara moja huko mbinguni, sasa angeanza kuwapa watoto hapa duniani nafasi nyingine ya kufanya uchaguzi kati ya Mti wa Uzima na Mti wa Mema na Ubaya na fursa ya kusimamisha tena Ufalme Wake. Kristo kupitia mwili wake uliounganishwa wa siku ya 8 watu anaanza kudhihirisha ushindi huu wa kimwili duniani leo!
Ninasema siku ya 8 kama imepita miaka elfu 2 tangu msalabani. Miaka elfu ni kama siku kwa Bwana, kwa hiyo wiki nzima imepita tangu uumbaji, na sasa tuko katika siku ya 8 katika majira ya Mungu.
2 Petro 3:8
8 Lakini, wapenzi, msisahau kitu kimoja, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.
Ni lazima tuwe na umoja, si tu kama familia ya kimwili, lakini muhimu zaidi roho zetu lazima zifungwe nira sawasawa katika ujuzi wa Mungu kwa sababu Kristo ni roho. Nafsi yetu mwanadamu hataweza kufahamu mwelekeo na mwongozo kupitia kwa Roho wake.
1 Wakorintho 2:13-14
13 Hayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa na hekima ya wanadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho na walio na huyo roho.
14 Lakini mwanadamu wa kidunia hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, kwa maana kwake huyo ni upuzi; wala hawezi kuzifahamu, kwasababu zatambulikana kwa jinsi ya rohoni
Ni lazima turuhusu roho zetu kukomaa katika sura yake kama watu binafsi, kisha kuungana kama familia ya kidunia ili kumfanya Yeye mwili kamili unaoonekana wa kufanya mazungumzo duniani, kuushinda ulimwengu huu kwa kutekeleza ushindi wake na kuleta kushindwa kwa ngome ya adui kwenye sayari. Hili ndilo kusudi Lake na utume wetu.
Shetani anataka tuwe na ugomvi kati yetu sisi kwa sisi na kwa Mungu. Je, unaweza kuona hili? Mpango wake ni kutuweka kuona na kufanya mambo ya kimwili, ya kiroho ili tusiweze kukua kiroho au kuelewa mambo ya kiroho. Nafsi zetu huona mema na mabaya, na ni wepesi sana kuona fursa mbaya inapowasilishwa kwetu. Shetani hata hivyo hawezi kumgusa au kumpotosha mwanadamu wetu wa roho, kwa hiyo ni lazima tutembee katika roho.
Kama dokezo la upande, kuwa mwangalifu sana. Ili kuufanya mwili wa Kristo usiwe na nguvu ni lazima tujihusishe na mambo ya ulimwengu huu. Shetani atakuvuta kwa maono ya mafanikio katika ulimwengu wake, au kuufuata, akiweka akili yako na nguvu zako zielekezwe kwenye eneo hili ambalo yeye ndiye mungu wake. Huwezi kuwa na nia ya Ufalme, au kukuza ukomavu wa mtu wako wa kiroho, ikiwa unakula mara kwa mara kwenye Mti wa Mema na Uovu, au unatafuta ushauri wa mwanadamu kulingana na akili ambayo imekuwa ikibadilika kutoka kwa mawazo ya Shetani tangu bustani.
Paulo alisema katika 2 Wakorintho 11:3:
3 Lakini naogopa kwamba, kama vile nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake ya uongo, fikira zenu zaweza haribiwa, mkauacha unyofu ulio ndani ya Kristo.
Paulo pia anapendekeza katika Waefeso 4:22-24,
22 kwamba mvueni, uhusiano na mwenendo wenu wa awali, yaani utu wa kale (utu wa nafsi) unaoharibika kulingana na tamaa zenye udanganyifu (fedha, mafanikio, mamlaka n.k.),
23 na kufanywa upya katika roho ya nia zenu,
24 mkavae utu mpya (mtu wa roho) ulioumbwa kulingana na Mungu, katika haki na utakatifu wa kweli.
Kwa hiyo tunaweza kuona ikiwa tunajihusisha na mambo ya ulimwengu huu, tukiwa na wazo la kufanikiwa kwa sababu nyingine yoyote zaidi ya kuendeleza masilahi ya Ufalme, tutabaki kuwa watu wa kimwili. Kwa bahati mbaya kama mwili wa kimwili, tukifanya mambo kwa njia yetu, kwa ajili ya kujiimarisha kibinafsi, udhibiti wa Shetani umehakikishwa. Tunajikuta tumepingana na Mungu na tunaweza hata kuanza kutopenda wale wanaotembea katika Roho. Hebu turejee sasa kwenye somo letu la asili, ushindi wa Kristo.
Baada ya kushinda pigano la kupata tena Ubwana wa sayari hii, Yesu alianza kuunda serikali yake mwenyewe ili kupigana na ulimwengu wa Shetani, akitimiza unabii ulio katika Isaya 9.
Isaya 9:6-7
6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto kiume; na ufalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
7 Maongezeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho, juu ya kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya ufalme wake, ili kuistawisha na kuimarisha kwa hukumu na haki, tangu wakati huo na hata milele. Bwana wa majeshi utatimiza hayo.
Kupitia Mitume na Manabii Wake, Yeye huleta kifuniko kwenye ardhi ili adui aweze kuzuiwa huku watu wake wakifikiwa na ukweli kutoka kwenye Mti wa Uzima. Baada ya kufundishwa, lazima pia kufunikwa na kulindwa. Vinginevyo adui atawanyang'anya mbegu za ukweli na badala yake kupanda mbegu za akili na mafundisho ya uongo, ambayo yangewasukuma kurudi moja kwa moja kwenye Mti wa Mema na Mabaya.
Akitumia wahudumu Wake watano Ataunda serikali Yake kuongoza na kuelekeza familia Yake kwenye ujuzi wa jinsi ya kujenga Ufalme Wake, na kusimamisha Dunia Mpya. Ujuzi huu hautatokana na hekima ya ulimwengu huu.
1 Wakorintho 2:5-7 inaeleza,
5 kwamba imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.
6 Hata hivyo, twanena hekima miongoni mwa wale waliokomaa, lakini si hekima ya ulimwengu huu, wala ya watawala wa ulimwengu huu, ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
7 Lakini twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu mwanzo kwa utukufu wetu,
Paulo kwa kweli anatuambia katika 1 Wakorintho 3:19-20 hekima ya ulimwengu inapingana na Mungu na ni ubatili. Kwa nini, kwa sababu ujuzi huu ni wa mungu wa dunia hii.
1 Wakorintho 3:19-20
19 Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, “Yeye huwanasa wenye hekima katika hila zao wenyewe;
20 na tena, “BWANA anayajua mawazo ya wenye hekima, kwamba ni ubatili.”
Wacha tufunge na mawazo haya ya mwisho. Ufalme mpya hauwezi kujengwa juu ya mawazo ya zamani. Mungu anaachilia Hekima kwa enzi hii ili kuanzisha dunia mpya. Sasa akili zetu za asili ni kama kiungo chochote katika miili yetu, ni sehemu tu ya utu wetu. Ni kile kinachoingizwa katika akili zetu ndicho kinacholeta tofauti. Fikiria akili yako kama kompyuta. Ikiwa maarifa mengi uliyokusanya yalitoka katika akili za mwanadamu, shule, chuo nk. hifadhidata yako imekusanywa kutoka kwa Mti wa Mema na Uovu. Ulimwengu huu unamilikiwa na Shetani. Ili kuwa sehemu ya yale ambayo Bwana anafanya, ni lazima tusugue akili zetu, tufute data hii duni na kuruhusu Roho Mtakatifu kujenga hifadhidata kamili ambayo roho zetu zinaweza kufanya kazi kutoka kwao.
Warumi 12:2 inatuonya:
2 Wala msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali mfafanywe upya kwa kuzibadili fikra na nia zenu, muweze kujua kwa hakika mapenzi ya mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
Na kuweza kuingia katika mpango wa Mungu.
Bofya vichwa ili kucheza nyimbo zinazohusiana na mada hii
You Can't Bring Condemnation
Victory Song
New Heaven New Earth