Scroll To Top

Mungu Ana Mpango

Sehemu ya Nne ya Mfululizo huu

Na Jacquelyn Fedor

Ilitafsiriwa Na David Odhiambo
2010-05-03


Tafadhali bofya maandishi ya samawati hafifu kwa maelezo zaidi


Kama ilivyoelezwa katika mlipuko wa juma lililopita, Yesu alimshinda Shetani kama inavyothibitishwa na kaburi tupu, na Bibi-arusi Wake, kanisa Lake, likafunguliwa ulimwenguni. Sasa Ataifufua nyumba Yake, na kuondoa uharibifu ambao adui aliuleta kwake, na kwa hakika, viumbe vyote hatimaye vitawekwa huru na kurejeshwa.
Warumi 8:21
21 kwa sababu viumbe vyenyewe navyo vitakombolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu na kuingia katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
Roho wake alikuja kulitia nguvu kanisa kwa ajili ya huduma siku ya Pentekoste. Viongozi waliojazwa na Roho waliinuliwa ili kuwazoeza waliozaliwa mara ya pili, na Roho Mtakatifu Mwenyewe humzoeza mwanadamu wetu wa kiroho, akiwapa asili yake, uwezo wake na ujuzi Wake.
1 Wakorintho 12:7-10 inazungumza juu ya jambo hili hili.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote;
8 kwa maana mtu hupewa neno la hekima katika Roho, na mwingine neno la maarifa katika Roho yeye yule;
9 na mwingine imani kwa yeye huyo Roho, kwa mwingine karama za uponyaji kwa Roho huyo,
10 kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii, kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na mwingine tafsiri za lugha.
Watu wote wa nyumba ya Mungu hivi karibuni watazungumza lugha moja ambayo imetokana na ujuzi wa Mti wa Uzima. Kwa hiyo utamaduni utabadilika, mifumo inayoendesha ulimwengu itabadilika vile vile tunapoanza kutembea katika roho pamoja Naye. Ni Yeye ambaye anaunganisha roho zetu za kibinadamu na ikiwa tutamruhusu atuzoeze na kutukamilisha, na kutuweka kila mahali tunapohusika katika mwili, mwili hivi karibuni utakuwa kimo kamili cha Kristo. Kazi kubwa zaidi tutazifanya kuliko Yeye alivyofanya kama mtu mmoja.
Yohana 14:12
12 “Amin, amin, nawaambia, Yeye aniaminiye Mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya (kama mtu binafsi); na kubwa kuliko haya atafanya (kwa sababu ni mwili wote wa Kristo), kwa sababu mimi naenda kwa Baba Yangu.
Alirudi mbinguni na akawa kiumbe wa roho tena. Sasa anaweza kuja katika mavazi mengi ya mwili ili kutimiza malengo Yake ya kidunia. Kristo ndani yetu anaweza kurejesha, si tu watu katika eneo moja kama alipotembea duniani, lakini ulimwengu wote unaweza kufaidika. Soma kile alichoweza kufanya katika injili na kisha umwone akifanya hivyo kupitia kwa familia Yake kote ulimwenguni! Hakika ni Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu.
Wakolosai 1:27
27 Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii kati ya mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
Tangu anguko la Adamu hadi kifo cha Kristo, mwanadamu aliachwa kwa hiari yake mwenyewe jinsi ya kuishi kwa sababu ya chaguo alilofanya Hawa kudhibiti hatima yetu wenyewe. Mungu angempa mwanadamu wakati mwingi wa kuona kwamba hawawezi kuishi kwa mafanikio bila Muumba wao. Yesu alisema wazi katika Yohana kwamba hatuwezi kuishi bila Yeye. Hatimaye, tunaanza kuona na kuelewa hili kweli!
Yohana 15:5
5 “Mimi (Yesu) ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Wale katika Dini ya Kiyahudi na kanisa la kale pia, walijaribu kutembea katika umoja na Mungu kadri walivyoweza, bado wakiendelea kufanya mambo kwa njia yao wenyewe, wakifanya mipango yao wenyewe. Tunajua bila shaka, hii haikufaulu, wala haiwezi kuwa hivyo. Tangu Kristo alipofufuka, mwanadamu alipewa nafasi ya kuingia katika pumziko lake. Angeweza kuishi kupitia mpango wa Mungu, hivyo kazi zake hazingekuwa tena kazi mfu zilizokamilishwa kupitia nguvu na akili yake mwenyewe.
Yeremia 17:5
5 BWANA asema hivi, “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
Kilichofananisha hili kwa mwanadamu ni kitambaa kilichokunjwa ambacho kilikuwa kimetumika kuficha uso wa Bwana kaburini. Haikuwekwa pamoja na zile nguo zingine za kaburini, bali ilikunjwa yenyewe ili kuvuta usikivu wa wale waliokuja kaburini kuuhudumia maiti yake.
Yohana 20:7
7 na ile kitambaa iliyokuwa kichwani mwake, hakikuwa Pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
Alikuwa anajaribu kutuonyesha nini? Ilimaanisha nini? Hebu tuangalie kwa karibu. Kinachofafanuliwa katika andiko hili kama "kitambaa" kwa hakika, kulingana na Strongs, kamusi ya Kigiriki, kitambaa cha jasho. Baada ya kuinuka, aliikunja vizuri na kuiweka kando. Je! Hakuwa akimwonyesha mwanadamu kwamba hangelazimika tena kuhangaika na kujitafutia mambo mwenyewe?
Waebrania 4:9-10
9 Basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu.
10 Kwa maana aingiaye katika pumziko yake atapumzika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.
Labda alitaka tuelewe, Mungu ana mpango kwa kila mmoja wetu na tukipenda, Mungu mwenyewe ataona kwamba tunatimiza hatima yetu. Kitambaa kilichokunjwa kiliashiria kwamba Yesu alikuwa amedhihirisha kwa ufanisi sehemu yake katika mpango wa Mungu kwa urejesho wa dunia na alikuwa ametimiza matakwa ya Mungu kuhusu wanadamu. Ilikuwa imekamilika. Alitimiza yote ambayo yalipangwa afanye tangu kuwekwa msingi wa dunia.
Bado, kukunja kwa kitambaa kulikuwa na maana nyingine pia. Ilikuwa ni mfano wa kuondolewa kwa sehemu hiyo ya laana ya mwanadamu ambayo Mungu alikuwa amesema juu ya Adamu kwa ajili ya kutotii kwake, akisema kwamba angelazimika kutoka jasho na kutaabika ili kula.
Mwanzo 3:17-19
17 Kisha akamwambia Adamu, “Kwa kuwa umemsikiliza mkeo, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, “Usile matunda yake”; ardhi imelaaniwa kwa kosa lako; kwa taabu utakula katika siku zote za maisha yako.
18 Miiba na michongoma itakuzalia, nawe utakula mimea ya shambani.
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, mpaka utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”
Kwa hiyo unaona, kwa sababu Kristo alitimiza mambo yote yaliyotakiwa kwake kabla ya msalaba, kisha pale msalabani, na sasa, ni Kristo kupitia kwetu, tunachopaswa kufanya ni kupumzika katika mpango wa Mungu. Hili linapaswa kuwa rahisi sana, lakini je, tunaingiaje katika mpango wa Mungu? Unaona, tunapozaliwa mara ya pili roho zetu zinaunganishwa moja kwa moja na nia ya Kristo. Tunaweza kuwa watoto wachanga hadi kujua jinsi ya kutembea hivi. Lakini inaweza kufanyika kwa urahisi “ikiwa” tunaweza kupumzika, kuingia katika pumziko Lake, na kwa hakika kuamini kwamba Mungu anatupenda na anajali vya kutosha kutuelekeza. Atafungua milango hakuna mwanadamu awezaye kufunga, atatengeneza mazingira ambayo hatuna uwezo wa kuyaumba. Adamu kwa mfano, kabla ya anguko, alitaja aina zote tofauti za viumbe, kwa sababu aliunganishwa kupitia roho yake kwa nia ya Kristo. Tuna uwezo huo leo tunapozaliwa mara ya pili, lakini itahitaji imani katika Mungu na kujizoeza kutumia uwezo huu na kupumzika katika ahadi yake ya kuingilia kati kwa niaba yetu.
Anatimiza mambo yote yanayotuhusu. Hata hivyo, kwa kweli ni vigumu kuamini\ upendo wa Mungu baada ya miaka hii yote ya kufichuliwa na ukatili wa Shetani. Asili ya Shetani kupitia roho ya mwanadamu imekuwa mfano wetu kwa maelfu ya miaka, lakini lazima sasa tuelewe, msalaba ulirekebisha hilo kwa wale wanaotaka kuanza upya. Hakika Mungu ni Mungu wa Upendo na hataki chochote ila bora kwa familia yake. Makosa yetu yamefunikwa, hatima yetu hakika.
Paulo alisema hivi katika Warumi 8:38 na 39.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenyemamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote, ataweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Ni lazima sasa tujifunze kudhihirisha ushindi wa msalaba na kuwa tayari kubadilika kutoka kwa njia tuliyotembea kabla ya kukutana na Kristo. Ni lazima tujifunze kupumzika kutokana na kazi zetu ili kupatana na mpango wa Mungu.
Waebrania 4:11
11 Basi na tufanye bidii kuingia katika pumziko hiyo, ili yeyote miongoni asije akaanguka kwa mfano huo wa kutomitii (wa Israeli wa kale).
Kwa kumalizia, ikiwa tunaweza kuwa watiifu ili kupumzika katika kazi ya Mungu, ni mpango Wake uliofunuliwa kuinua watu Anaoweza kukaa ndani yao na kuishi ndani yao ili kuanzisha mzunguko mpya au enzi kuwa. Watoto wa siku ya 8! Yote ni sehemu ya mpango Wake.
Bofya vichwa ili kucheza nyimbo zinazohusiana na mada hii
Hybrid Seed
Christ In Us
A Brand New Day